SHILOLE: SIONI AIBU KUONGEA KIINGEREZA CHA KUBABAISHA

12:54 AM
Shilole’ amesema kuwa haoni aibu kuzungumza lugha ya Kiingereza kwa makosa akidai kuwa anafanya hivyo kama njia mojawapo ya kujifunza kutokana na makosa.

Alisema, Kiingereza sio lugha mama ya Mtanzania hivyo haoni taabu kuongea ‘broken English’ na kwamba anajitahidi kufahamu kadri anavyoweza.

Video za Shilole akizungumza Kiingereza cha kuchapia zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii na kuwa burudani kwa watu wengine.

“Si mnaonaga wenyewe muda mwingine nisipoongea Kiswanglish changu watu wanaanza kunitafuta… ooh Shishi tafadhali ongea bhana, tunataka uongee,”alisema shilole alipokuwa akizungumza na kituo kimoja cha radio

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »