NEY WA MITEGO AFUNGUKA-SIFANYI MUZIKI KWA AJILI YA TUZO

4:37 AM
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa Mitego ambaye alisumbua sana na wimbo wake 'Shika adabu yako' ambao ulifungiwa na Baraza la Sanaa (BASATA)

na sasa ameachia wimbo wake mpya 'Saka hela' amefunguka na kusema kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata au kushinda tuzo..

Nay wa Mitego aliyasema haya alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha eNEWS na kuwataka mashabiki wa muziki wake watambue kuwa yeye hafanyi muziki ili kupata tuzo au kushinda tuzo bali yeye anafanya muziki kutoa burudani, kurekebisha sehemu anapoona si sawa pamoja na kumuingizia kipato ndiyo maana siku zote huwa anajiita mwanamuziki mfanyabiashara.
"Mimi siku zote sifanyi muziki ili nipate tuzo au nishinde tuzo hata mashabiki zangu naomba mtambue kuwa mimi sifanyi muziki kwa ajili ya tuzo" alisema Nay wa Mitego.

Katika hatua nyingine Nay wa Mitego anadai kuwa anapotoa ngoma zake za kuchana watu au kurekebisha baadhi ya mambo kwa watu au jamii huwa zinapokelewa vizuri zaidi na kuleta changamoto kwenye muziki ikiwa pamoja na kuchangamsha muziki wa bongo

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »