MORINHO KUFANYA USAJILI WA KUFA MTU MAN UNITED

11:15 PM
Kocha ajae Manchester United, Jose Mourinho anategemewa kufanya mageuzi makubwa kwenye kikosi cha timu hiyo kwa usajili wa wachezaji nyota utakaoigharimu timu hiyo takriban pauni milioni 200 katika msimu huu wa usajili.
 Mourinho anayeenda kuchukua mikoba ya Louis van Gaal aliyetimuliwa Jumatatu, amewakeka katika orodha yake sentahafu John Stones wa Everton na kiungo wa Chelsea Nemanja Matic. Stone anatarajiwa kuigharimu Manchester United pauni milioni 45 wakati Matic anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25. 
Mourinho pia anampigia hesabu beki wa Real Madrid Raphael Varane mwenye thamani ya pauni milioni 45 pamoja na kiungo bab kubwa wa Sporting Lisbon ya Ureno Joao Mario kwa pauni milioni 35. Kama vile hiyo haitoshi, Mourinho anatarajiwa kuimarisha safu ya ushambuliaji ya United kwa kumulika wachezaji kadhaa akiwemo muuaji mkongwe wa PSG Zlatan Ibrahimovic, Alvaro Morata wa Juventus na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid. 

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »