Beki wa Arsenal Hector Bellerin ameitwa katika kikosi cha Timu ya Taifa ya Hispania kukamilisha kikosi cha wachezaji 23 watakaowakilisha Taifa hilo katika michuano ya Euro 2016,
Nafasi hiyoimekuja baada ya aliyekuwa beki wa kutumainiwa katika nafasi hiyo Dani Carvajal kuwa majeruhi ambayo aliyapata akiiwakilisha klabu yake ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid katika fainali ya UEFA Champions Ligue ambapo Real Madrid waliibuka mabingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.

Majeruhi hayo yanamfanya kukosa michuano hiyo mikubwa barani ulaya na nafasi yake kuchukuliwa na kijna huyo wa Arsen Wenger.
Kikosi cha Hispania cha wachezaji 19 kati ya 23 kimetangazwa asubuhi ya leo na kocha anatarajiwa kutangaza wengine wanne waliobaki hapo baadae