GENK YA SAMATTA YAUA 5-2, IKISHINDA MECHI YA MWISHO INAFUZU ULAYA

4:26 AM
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa kuamkia leo ameisaidia timu yake, KRC Genk kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa mchujo Ubelgiji kuwania kucheza michuano ya Ulaya. 
Samatta alicheza kwa dakika zote 90, mabao ya Genk yakifungwa na Leon Bailey dakika ya 45, Buffel dakika ya 65, Pozuelo dakika ya 76, Ndidi dakika ya 78 na Nikos Karelis dakika ya 90 na ushei wakati ya Anderlecht yalifungwa Filip Djuricic dakika ya 25 na Suarez dakika ya 60. 
Genk sasa itahitaji ushinda katika mchezo wao wa mwisho Jumapili dhidi ya Genk ugenini ili kufuzu moja kwa moja Europa League.

Club Brugge inaongoza mchujo wa kuwania michuano ya Ulaya kwa pointi zake 53, ikifuatiwa na Anderlecht yenye pointi 44, AA Gent pointi 41 na Racing Genk pointi 39.
Timu itakayomaliza katika nafasi ya nne, ili kupata tiketi ya kucheza Europa League italazimika kumenyana na mshindi kati ya Charleroi na Kortrijk zitakazomenyana katika mchezo mwingine wa mchujo. 

Samatta jana amecheza mechi ya 15 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
Katika mechi hizo, ambazo nane tu ndiyo ameanza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »