#AUDIO: Dada wa Marehemu Aneth Msuya kasimulia mkasa mzima wa mauaji ya Kinyama ya mdogo wake

1:14 PM
May 30 2016 kupitia Hekaheka ya Clouds FM Geah Habib ametuletea hii ya Dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya ambaye aliuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake jijini Dar es salaam. Kama hukupata time ya kuisikiliza hii usijali imekurekodia full stori kutoka kwenye Hekaheka ya leo.
Geah alifika nyumbani kwa marehemu na akazungumza na majirani na mjumbe ambao wanasema kwamba hawakusikia chochote kama vile kelele lakini walipata baadae taarifa kwamba jirani yao ameuawa. Mmoja wa majirani amezungumza kwamba alimuona marehemu akiwa nje ya geti amekaa ndani ya gari muda mrefu sana.

>>>siku hiyo ilikuwa saa tisa huyo mama alisimama getini na gari lake sikujua alikuwa anasubiri nini, nikapita zangu, asubuhi nakuja hapa kwenye kazi yangu nakuta watu wamekusanyika na baadae polisi wakaja:-Jirani

Geah amezungumza pia na Dada wa marehemu Aneth Msuya ambapo ameyazungumza haya……….

>>>‘wamemkata hadi koromeo, ni unyama gani unafanyika Tanzania, 2013 wamemuua kaka yangu Erasto Msuya, mwezi wa 12 wamempiga mdogo wangu risasi na mme wake wameenda kuponea Aga khan jiulize kuna nini’
STORI KAMILI BONYEZA PLAY HAPA CHINI NIMEKUWEKEA…

Share this

SPORT HITS IS A BLOG BASED ON PROVIDING SPORT NEWS FROM ALL AROUND THE WORLD, STAY WITH US ALL THE TIME FOR INSTANT UPDATES.. Dont Forget to follow us on Facebook, twitter and Instagram @sporthitstz

Related Posts

Previous
Next Post »